Mikoa
18 kati ya 27 ya kimpira tayari imeshapata mabingwa wao kwa ajili ya
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa itakayoanza Mei 12 mwaka huu chini ya
usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Timu
tatu za juu katika Ligi hiyo ya Mabingwa zitapanda daraja kucheza Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao (2013/2014). Ligi ya FDL ina jumla ya
timu 24 ambapo tatu katika ligi hiyo zilizoshuka daraja msimu huu ni
Moro United ya Dar es Salaam, Small Kids ya Rukwa na Morani FC ya
Manyara.
Mabingwa
waliopatikana hadi sasa na mikoa yao kwenye mabano ni Abajalo SC (Dar
es Salaam 2), Biharamulo FC (Kagera), Flamingo SC (Arusha), Friends
Rangers (Dar es Salaam 3), Katavi Warriors (Katavi), Kiluvya United
(Pwani), Kimondo FC (Mbeya) na Machava FC (Kilimanjaro).
Wengine
ni Magic Pressure FC (Singida), Mbinga United (Ruvuma), Mji Njombe
(Njombe), Polisi Jamii Bunda FC (Mara), Red Coast FC (Dar es Salaam 1),
Rukwa United (Rukwa), Saigon FC (Kigoma), TECKFOLT FC ya Kilombero
ambayo ni Shule ya Sekondari (Morogoro) na UDC FC ya Ukerewe (Mwanza).
Kila
klabu inatakiwa kulipa ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000 wakati
usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika Ligi ya
Mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF
inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya
ligi hiyo.
MTANZANIA AOMBEWA ITC ACHEZE NORWAY
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Norway (NFF) limetuma maombi ya kupatiwa Hati ya
Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Mtanzania Godfrey Mlowoka ili
aweze kucheza mpira nchini humo.
NFF
inamuombea hati hiyo Mlowoka ili aweze kujiunga na klabu ya Ekne IL
kama mchezaji wa ridhaa ambapo klabu yake ya zamani aliyokuwa akiichezea
nchini imetajwa kuwa Sadani.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara
taratibu zote zitakapokamilika hati hiyo ya uhamisho itatumwa nchini
Norway.
AZAM YAENDELEA KUJINOA MOROCCO
Timu
ya Azam ambayo iko jijini Rabat kwa ajili ya mechi ya marudiano ya
raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabati ya huko
inaendelea vizuri na mazoezi.
Kwa
mujibu wa Ofisa Habari Msaidizi wa Azam FC, Jaffer Idd maandalizi
yanakwenda vizuri kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Mei 4
mwaka huu). Jaffer Idd anapatikana kwa namba +212671146092.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment