ni hatari lakini haina jinsi, kushoto ni mwandishi wa habari wa ebony fm akiwa katika usafiri wa toyo.
hali halisi ndio kama hivi
hapa ni eneo la posta ambapo huwa zinapaki daladala lakini leo usafiri ndio huu na wapiga debe wapo kama kawaida.
mamia ya abiria na wasafiri katika eneo la stand ya miomboni asubuhi ya leo
mmoja wa madereva akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa star tv oliver motto na clement sanga wa chanel ten
hapa ni eneo la stendi ya miomboni ambapo huwa zimejaa daladala lakini siku ya leo hadi muda huu wa saa nne hakuna daladala hata moja.
JESHI la polisi likimuondoa afisa wa sumatra aliyekuwa akifanyiwa mahojiano katika kituo cha radio ebony fm, ambapo madereva wakiwa na hasira waliandamana hadi nje ya kituo hicho wakitaka kumfanyia fujo.
madereva hao wameingia kwenye mgomo kwa madai ya kupinga kuzuiwa kupaki katika kituo cha daladala cha miomboni na posta na badala yake wakitakiwa kushusha abiria na kuendelea na safari.
hatua hiyo ya kuzuiwa kupaki katika vituo hivyo imekuja kufuatia malalamiko ya abiria kujikuta wakilipa nauli mara mbili katika safari moja mfano kutoka frelimo hadi tumaini.
mtandao huu utaendelea kukuletea yatakayojiri
0 comments:
Post a Comment