kuanzia kushoto ni afisa mfawidhi wa sumatra, rto, salim asas, madam jesca, na ocd katika kikao na maderva wa daladala
Baada ya saa tisa ya mgomo wa madereva wa daladala manispaa ya iringa, hatimaye hali ya usafiri imerudi katika hali yake ya kawaida baada ya kikao kilichowahusisha wadau wa usafirishaji.
Kikao hicho cha wadau kilichokutana katika ukumbi wa hallfear , kimewakutanisha madereva, makondakta, mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani, kamanda wa kikosi cha usalama barabarani , mwakilishi wa manispaa na sumatra.
Katika kikao hicho madereva wameelekeza lawama nyingi sumatra na kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa taasisi hiyo kwa faini zake kutoeleweka, manispaa kutoeleweka katika upangaji wa vituo na kuweka ushuru mkubwa .
Hata hivyo baada ya majadiliano ya muda mrefu wadau hao wamekubaliana kurudisha huduma kama kawaidi kwa kurudishwa vitu vilivyoshikwa sambamba na kuachiwa magari yaliyokamatwa.
Kwa upande wake kamanda wa usalama barabarani mkoa wa iringa Pamphil g Honono amesema utaratibu uliokuwepo uendelee kama kawaida kwa madereva na makondakta kuwajali wateja wao na kuwaepusha na kero.
Akizungumza na wanahabari baada ya kikao hicho afisa mfawidhi sumatra mkoa wa iringa Rahim Kondo amesema changamoto hizo ni zakawaida katika utendaji.
akifunga kikao hicho mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Salim Abri amesema kuanzia sasa viongozi wa daladala watakua na mwakilishi katika kamati hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa kikao cha wadau kwa ajili ya kuzijadili changamoto zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment