Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya
Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la
shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili
wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, kukatiza ziara
hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu
na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la
kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo
wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo
la Ahmadi mjini Kuwait.
Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha
jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa
Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment