Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea kesho (Aprili 13 mwaka
huu) kwa mechi mbili zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa
Taifa wakati Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania
Prisons na Ruvu Shooting.
Ligi hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 14 mwaka huu)
kwa mechi kati ya wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
WASHELISHELI
KUICHEZESHA AZAM CAF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua
waamuzi kutoka Shelisheli kuchezesha mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe
la Shirikisho kati ya Azam na AS FAR ya Morocco itakayofanyika Aprili 20 mwaka
huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi hao ni Emile Fred atakayepuliza filimbi
akisaidiwa na Steve Maire na Jean Ernesta. Mwamuzi wa mezani (fourth official)
atakuwa Jean Claude Labrossa. Kamishna wa mechi hiyo ni Abbas Sendyowa kutoka
Uganda.
Wakati huo huo, CAF imemteua Mtanzania Alfred Lwiza
kuwa Kamishna wa mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati
ya Liga Muculmana ya Msumbiji na Wydad Casablanca ya Morocco.
Mechi hiyo itakayochezwa kati ya Aprili 19,20 au 21
mwaka huu nchini Msumbiji itachezeshwa na waamuzi kutoka Zimbabwe wakiongozwa
na Ruzive Ruzive.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment