Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko za kifo cha
Mkuu wa zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Makame
Rashid kilichotokea juzi (Aprili 14 mwaka huu) kutokana na maradhi
jijini Dar es Salaam.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga amesema msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira
wa miguu kutokana na mchango aliotoa Meja Jenerali Makame Rashid ikiwemo
kuwa mlezi wa timu ya Ruvu Stars wakati huo akiwa Kamanda (CO) wa
Kikosi cha Ruvu JKT.
Pia
aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mdhamini
(Trustee) wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania
(FAT) na wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika miaka ya themanini
alikuwa sehemu ya mafanikio kwa timu ya Tukuyu Stars ya Mbeya iliyotwaa
ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1987 ikiwa ndiyo kwanza imepanda kucheza
Ligi Kuu wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Meja Jenerali Makame Rashid, Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya
Olimpiki Tanzania (TOC), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko
yanatarajiwa kufanyika leo (Aprili 16 mwaka huu) nyumbani kwao mkoani
Mtwara. Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi. Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment