Main Menu

Wednesday, April 17, 2013

BUNGE LAENDELEA KUVURUGWA, TINDU LISSU AGOMA KUTOLEWA BUNGENI, TBC YASITISHA MATANGAZO.



Televisheni ya taifa TBC jioni ya leo imelazimika kukatisha matangazo ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya naibu spika wa bunge hilo Job Ndugai kuwataka polisi kumtoa mbunge wa Singida mashariki Tindu Lissu baada ya kuomba muongozo wakati mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba alipokua akichangia makadirio ya bajeti ya ofisi ya Rais iliyowasilishwa leo.

Muongozo wa Tindu Lissu ulikuja baada ya Mwigulu Nchemba kusema kuwa dr Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 mkoani Singida wakati wa kufanya mkutano wa ndani aliwakusanya viongozi wa dini ya Kikristo badala ya wanachama wa chama chake hali iliyosababisha aliyekua mratibu wa kampeni kipindi hicho kusimama na kupinga taarifa hiyo ambayo Mwigulu aliikataa taarifa hiyo.

 

Baada ya mwiguru kuikataa taarifa hiyo ndipo Tindu Lissu alipoomba muongozo na spika wa Bunge kumkatalia kwa madai kuwa aliposimama kuzungumza hakuna mtu aliyemsumbua na kwamba amesimama mara nyingi kuomba muongozo hivyo awe mvumilivu hali iliyosababisha kutoelewana na ndipo Naibu spika alipoita askari kwa ajili ya kumtoa Tindu Lissu bungeni huku maneno ya kejeli na kashfa yakiendelea kutolewa na wabunge.
 

Kutokea kwa hali hiyo kulisababisha televisheni ya taifa kukata sauti kutoka bungeni huku picha zikimuonyesha Tindu Tissu akibishana na askari kutolewa bungeni na askari kwa ajili ya kutoa siwa akizuiwa na naibu spika kuitoa siwa wakati lisu akilumbana na askari, hata hivyo badae TBC  walisitisha matangazo ya bunge.

Sasa kilichotokea baada ya hapo mimi sijui .

Pia ikumbukwe kuwa mcha wa leo tarehe 17 april mbunge wa kigoma mjini Peter Selukindo alitukana bungeni na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa (oooh fu***k u) swali ni je hakusikika bungeni au sio kosa kutukana? maana hakuchukuliwa hatua yoyote.

0 comments:

Post a Comment