Main Menu

Wednesday, April 17, 2013

YANGA YABANWA MKWAKWANI NA MGAMBO SHOOTING

BAO la kujifunga la mgambo shootong katika dakika ya 90 jioni hii limeinusuru klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam kuzama kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya kulazimisha sare ya 1-1.

  Sare hiyo inamaanisha mbio za ubingwa bado zinaendelea kati ya Yanga SC yenye pointi 53 kileleni huku ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 47.

  Bao la kutangulia la Mgambo shooting lilipatikana katika dakika ya 42 likifungwa na Issa Kanduru baada ya kupokea pasi ya salum mlima aliyemzidi ujanja beki wa kati ya yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
  Mchezo huo uligawanyika katika sehemu mbili ambapo kipindi cha kwanza mgambo walitawala wakati kipindi cha pili yanga walitawala zaidi.

0 comments:

Post a Comment