Uhuru kenyatta rais wa nne wa kenya
Rais-mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto
wameonya kuwa Kenya haiwezi kumudu gharama za mishahara na hivyo
wamesema serikali yamkini ikakata mishahara hiyo au kusimamisha nyongeza
ya mishahara.
Wawili hao wakizungumza Jumatano wamesema huenda Kenya ikapoteza
nafasi yake ya kiuchumi barani Afrika kutokana na bajeti kubwa ya
mishahara.
Uhuru amesema serikali yake itajitahidi kupunguza bei za
bidhaa muhimu ili wakati mishahara itakapopunguzwa, Wakenya wawe na
uwezo wa kujidhaminia maisha bora.
Kwa upande wake makamu wa rais mteule William Ruto amesema Kenya
inatumia asilimia 12 ya Pato Ghafi la Ndani au GDP kugharamia mishahara
ya watumishi wa umma katika hali ambayo nchi zingine za Afrika kusini
mwa jangwa la Sahara hutumia chini ya asilimia saba ya GDP kulipia
mishahara ya watumishi wa umma.
Amesema hicho ndicho kiwango wastani
duniani ambacho huwezesha kuwepo ustawi endelevu.
Matamshi hayo yanakuja
siku moja baada ya Tume Inayoshughulikia Mishahara ya Maafisa wa Umma
Kenya kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 37 kutoka shilingi
850,000 hadi 532,500.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011, serikali ya
Kenya ina wafanyakazi takribani 220,000.
0 comments:
Post a Comment