Main Menu

Thursday, March 14, 2013

PAPA FRANCIS WA KWANZA ATAKIWA KUMALIZA KASHFA YA NGONO KANISANI

Papa francis wa kwanza 

Jumuiya ya Wahanga Walionyanyanswa Kijinsia Na Makasisi (SNAP) nchini Marekani imetoa wito kwa Papa Francis I aliyechaguliwa upya kulipa umuhimu mkubwa suala la kupambana na makasisi ambao wanahusika na kashfa za ngono katika Kanisa Katoliki.

Jumuiya hiyo ya waliodhalilishwa kijinsia na Makasisi wa Kikatoliki imetoa taarifa leo Alkhamisi ikisema Papa Francis wa Kwanza ana wajibu wa kuzuia kunajisiwa watoto wadogo ambao huhujumiwa na makasisi wenye usiri mkubwa katika kanisa hilo. 

Taarifa hiyo imesema wazazi wanaowapeleka watoto wao makanisani wana wasiwasi mkubwa kuwa wako katika hatari ya kudhalilishwa kijinsia na mkakasisi. 

Aidha wametaka Kanisa Katoliki lifichue majina ya makasisi wahalifu. 

Ikumbukwe kuwa makasisi wa Kikatoliki ambao wote huwa wanaume hawaruhusiwi kuoa katika kipindi chote cha maisha yao ya kuhudumia wadhifa huo. 

Imebainika kuwa makasisi wengi hawawezi kuvumilia hali hiyo jambo ambalo limepelekea kuongozeka kashfa za jinai za ngono kanisani. 

Jana Jumatano Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina alichaguliwa kuwa papa mpya wa Kanisa Katoliki na atajulikana kwa kifupi kama Papa Francis I.

chanzo radio tehran

0 comments:

Post a Comment