Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia
kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za
kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya
Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika
hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza
Januari 7 mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha
wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni
Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa
Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na
Shomari Kapombe (Simba).
Viungo
ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba),
Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na
Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji
ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas
Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali
ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh
(Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso
(Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda
(Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
CAF YAMTUMA LIUNDA KUKAGUA VIWANJA ETHIOPIA
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa wake Leslie Liunda wa
Tanzania kwenda Ethiopia kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa utaratibu wa utoaji leseni kwa klabu zitakazoziwezesha
kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa
huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari 2 mwaka huu) ambapo
anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 6 mwakani na baadaye kupeleka
ripoti yake CAF.
Utekelezaji
wa kazi yake hiyo nchini Ethiopia utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), Wizara ya Michezo ya
nchi hiyo, viongozi wa klabu na mameneja wa viwanja husika.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment