Tuesday, January 1, 2013
22 WAZALIWA MKESHA WA MWAKA MPYA MKOANI IRINGA
Wakati watu duniani kote wakiendelea na shamrashamra za kuupokea Mwaka mpya wa 2013, Jumla ya watoto 22 wamezaliwa katika Hospitali ya rufaa Mkoa wa Iringa, katika mkesha wa siku ya Mwaka mpya.
Akizungumzia ujio wa watoto hao, Ofisa muuguzi msaidizi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa, Edda Sanga amesema kati ya Watoto 22, wakike ni 16 na watoto wa kiume ni 6.
Wakiwa na nyuso za furaha akinamma waliopata watoto usiku wa kuamkia leo wameshukuru kwa kujifungua salama tena usiku wa siku ya mwisho ya mwaka na mwanzo wa mwaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment