Tuesday, January 1, 2013
MSANII WA FILAMU SAJUKI AFARIKI DUNIA JIJINI DAR ES SALAAM.
Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala,Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.
ikumbukwe taarifa za sajuki kuumwa tena zilianza kuripotiwa pale alipoanguka jukwaani mkoani arusha alipokua ameandaa tamasha kwa ajili ya kuwashukuru watanzania waliomchangia kipindi alipokua anaumwa na kufanikisha kupelekwa india kwa ajili ya matibabu.
wakazi wa mkoa wa iringa watamkumbuka zaidi sajuki kwani tarehe 25 mwezi wa kumi na moja 2012 alifanya tamasha la asante tanzania lililofanyika katika uwanja wa samora na kuhudhuriwa na wapenda filamu wengi wa mkoa huo.
mungu amlaze mahali pema sajuki na amtie nguvu mke wake wastara ambaye alikua anampenda sana mmewe na alimpigania kuhakikisha anapona na kurudi katika hali yake ya kawaida, pamoja na mtoto wake mdogo.
sajuki alikua amelazwa katika hospitali ya muhimbili kwa takribani wiki mbili na alikua akifanya utaratibu wa kupelekwa tena nchini india.
utaratibu wa mazishi utatangazwa hapo baadae endelea kufuatilia mtandao huu.
Sujuki katika tamasha la asante tanzania mkoani iringa
mungu amlaze mahali pema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment