SAKATA la kupinga ujenzi wa bomba la gesi inayovunwa katika
Kijiji cha Msimbati mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, limechukua sura
mpya baada ya maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara kujiandikisha katika
fomu maalumu kupinga mradi huo.
Tayari majina hayo yamekabidhiwa kwa Katibu wa
Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya kwa ajili ya
kuyawasilisha bungeni kama kielelezo halali cha wananchi hao kupinga
mradi huo, ambapo utaratibu wa wananchi hao kujiorodhesha uliandaliwa na
chama hicho.
Taarifa zinaeleza kuwa zaidi ya wakazi 30,000 wa Mtwara wamejiorodhesha kupinga mradi huo wa gesi.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye mkutano
mkubwa wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara
na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi kutoka wilaya zote tano ya mkoa
huo, ambao hawakujali mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
Watu wa kada mbalimbali waliliambia Mwananchi
Jumapili kwamba haijawahi kutokea umati mkubwa wa watu kuhudhuria
mkutano wa hadhara mkoani humo kama ilivyokuwa kwa mkutano wa jana.
Walisema kuwa idadi hiyo ya watu ni zaidi ya waliojitokeza katika maandamano ya kupinga mradi huo, yaliyofanyika Desemba 27 mwaka jana.
Walisema kuwa idadi hiyo ya watu ni zaidi ya waliojitokeza katika maandamano ya kupinga mradi huo, yaliyofanyika Desemba 27 mwaka jana.
Majina hayo yalikabidhiwa na makatibu wa CUF wa
wilaya za mkoani huo huku mwakilishi wao Saidi Kulaga, akisema kuwa
zaidi ya watu 30,000 wamejiandikisha kupinga mradi huo.
Alisema wananchi hao wanataka Serikali kujenga mitambo ya kufua umeme mkoani humo, ili kuinua uchumi wa mikoa ya kusini.
“Kwa niaba ya wananchi hawa na mbele yao,
nakukabidhi majina na sahihi zao, wakipinga mradi wa kusafirisha gesi
kwenda Dar es Salaam. Wazee wetu waliwaondoa wanyonyaji weupe, sasa ni
zamu ya vijana kuwaondoa wanyonyaji weusi,” alisema Kulaga huku
akishangiliwa na umati wa watu.
Akipokea fomu hizo, Sakaya alisema kuwa wabunge wa
CUF, wamesikia kilio cha wananchi wa Mtwara na kwamba watahakikisha
wanawasilisha katika Bunge lijalo.
Katika mkutano huo mabango kadhaa yalibebwa na baadhi yakisomeka: “Shemejiii gesi haitoki…: Kikwete tuachie gesi yetu.”
Kabla ya mkutano kuanza umeme ulikatika eneo hilo
hali iliyosababisha kundi la vijana kuivamia Ofisi ya Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco), mkoani humo wakiishinikiza urudishwe, kitendo
kilichowalazimu polisi kuingilia kati na kufyatua mabomu ya machozi ili
kuwatawanya wananchi hao.
Wananchi waliondoka eneo la ofisi hizo na kurudi
uwanja wa mkutano, ambapo baadaye na mkutano huo uliendelea kwa amani
na utulivu, huku polisi wakiwa katika tahadhari kubwa.
chanzo mwananchi.
chanzo mwananchi.
0 comments:
Post a Comment