Main Menu

Wednesday, July 22, 2015

YANGA YAFUFUA MATUMAINI KAGAME CUP YAICHAPA TELECOM 3 -0



Mabingwa mara tano wa michuano ya Kombe la Kagame timu ya Young Africans leo imefufua matumaini ya kutinga robo fainal ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya Telecom kutoka nchini Djibout, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Malimi Busungu aliyefunga mabao mawili, na Geofrey Mwashiuya  aliyefunga bao la tatu kwa kombora kali umbali wa mita 20 na kupeleka kilio kwa timu ya Telecom.

Katika mchezo wa leo Yanga walipoteza penati mbili zilizopigwa na washambuliaji wake Amissi Tambwe na Saimon Msuva katika kipindi cha kwanza.
  
Katika mchezo wa uliotangulia mapema saa 8 mchana, timu Khartoum ilibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya KMKM, huku katika uwanja wa Karume KCCA ya Uganda ikiibuka na ushindi wa bao 1-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.

0 comments:

Post a Comment