Main Menu

Saturday, May 16, 2015

SADIO MANE AWEKA REKODI YA KUFUNGA HAT TRICK YA HARAKA ENGLAND



Southampton's Sadio Mane celebrates the first of the first-half treble on his way to the fastest ever Premier League hat-trickMshambuliaji wa Southampton Sadio Mane ameweka rekodi ya kufunga magoli matatu ya mapema katika historia ya Ligi Kuu ya soka nchini England.

Mane amefunga magoli hayo ndani ya dakika 2 na sekunde 56.

Magoli hayo matatu ya Mane yanamfanya mchezaji huyo kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Robbie Fowler ya kufunga magoli matatu ndani ya dakika 4 na sekunde 33.

Fowler alifunga magoli hayo katika mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal.

Ila wawili hao wanaweza wasijivunie sana kwani katika historia ya  soka nchini England, hat trick ya mapema kabisa ni ile aliyofunga James Hayter katika mchezo wa Ligi daraja la pili mwaka 2004 kati ya timu yake ya AFC Bournemouth na timu ya Wrexham.

Katika mchezo huo Hayter alitumia muda wa dakika 2 na sekunde 20 kufunga magoli matatu.
Alan Hutton is helpless as Mane slots in his first of the day with a simple left-footed finish after a defensive shambles from Villa
Mane makes it 2-0 little more than a minute after his first with his other foot, again into an unattended net 
Mane's third was a gem of a finish, first time with the side of his right boot and into the roof of the net

0 comments:

Post a Comment