Baadhi ya makocha wakiwemo wachezaji
wa zamani wakifuatilia mafunzo ya ukocha ngazi ya pili.
Kocha mkuu wa Twiga Stars, Rogasian
Kaijage akitoa somo kwa makocha wanashiriki kozi ya ukocha ngazi ya pili ndani
ya darasa kwenye Ukumbi wa Harbours Club, Kurasini.
Kocha mkuu wa Twiga Stars akitoa somo
kwa makocha wa kozi ya ngazi ya pili kwa vitendo
KOZI ya makocha wa ngazi ya pili
(Intermediate) inayosimamiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA), inatarajiwa kufungwa Jumanne ijayo baada ya kudumu kwa wiki nne.
Kozi hiyo ilianza Juni 3 mwaka huu
kwenye Ukumbi wa Harbours Club, uliopo Kurasini chini ya Mkufunzi Rogasin
Kaijage, ambaye ni Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ ambapo
makocha mbalimbali pamoja na wachezaji wa zamani wamejitokeza kushiriki.
Ofisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo
alisema kozi hiyo imekuwa na mafanikio na wanatarajia makocha walioshiriki
katika kozi hiyo watakuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu
katika mkoa wa Dar es Salaan na Taifa kwa ujumla.
“Hadi sasa tunashukuru kuona
tunafanikisha kozi hii ambayo wengi wameitikia wito, mwisho wa kozi hii ndio
mwanzo wa kozi nyingine.
“Lakini haya ya kozi ya makocha ni moja
ya majukumu ya Kamati ya Ufundi ya DRFA yaliyoainishwa katika Katiba, hivyo
hili ni moja ya shabaha yetu na mengine mengi mazuri yanafuata,” alisema
Mharizo.
Kozi hiyo ni ya kwanza kuendeshwa
na DRFA tangu kuingia madarakani kwa uongozi mpya wa chama hicho Desemba 12,
chini ya Mwenyekiti wake Almas Kassongo.
0 comments:
Post a Comment