Main Menu

Tuesday, April 30, 2013

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA JANUARI HADI APRIL 2013 WILAYA YA KILOLO MKOANI IRINGA




                            mkuu wa wilaya ya kilolo gerald guninita



UTANGULIZI


Wilaya ya Kilolo ina eneo la kilometa za mraba zipatazo  7,881 ikiwa Kilometa za mraba 5,331 zinafaa kwa Kilimo na shughuli za Ufugaji,  eneo la Kilometa za mraba 2,550 ni eneo la  misitu ya asili,  milima na hifadhi za wanyama. Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ilionyesha Wilaya ilikuwa na watu 218,227 kati yao  wanawake ni  112,622  na wanaume  ni 105,605 .Wilaya ya Kilolo  kiutawala ina Jimbo 1 la Uchaguzi  (Jimbo la Kilolo), Tarafa 3,  Kata  22, Vijiji 106, Vitongoji  555 na Kaya 51,455.

HALI YA ULINZI NA USALAMA
Kwa kipindi hiki cha January - April  2013, Hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yote ya Wilaya inaendelea kuwa ya amani na utulivu .Hakuna matukio makubwa yaliyosababisha wananchi kushindwa kuendelea na shughuli za maendeleo na kijamii. Matukio madogomadogo ya uhalifu yaliendelea kudhibitiwa na vyombo vya dola kikamilifu.

UTAWALA BORA
Wilaya imeendelea kuendesha shughuli zake za kiutawala na kisiasa ambapo mambo yafuatayo yamefanyika
·         Vyama vya siasa vimeendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu.
·         Kuendesha vikao vya kamati mbalimbali zilizoko Wilayani kama ifuatavyo:- Kikao cha kamati  ya wataalamu wa Wilaya, kamati ya Fedha  mipango na utawala, kamati ya Elimu Afya na maji, kamati ya uchumi , ujenzi na mazingira, kamati ya maadili ya Wilaya na Baraza la madiwani  tarehe 24/04/2013
·         Kikao cha kamati ya maadili ya mahakama Wilaya kimefanyika tarehe 14/03/2013 na kuazimia  kuwa elimu itolewe kwa wananchi juu ya umuhimu wa kamati hii na taarifa hii iwafikie wananchi   kupitia Waheshimiwa Madiwani na watendaji, ambapo katika kikao cha Baraza la madiwani 24/04/2013  ujumbe huo ulitolewa katika Taarifa ya Serikali na Mkuu wa Wilaya.
·         Serikali iliendelea kuwahimiza viongozi wa Serikali za Vijiji kuhakikisha mikutano mikuu ya Vijiji inafanyika kila baada ya miezi mitatu na kuwasomea wananchi mapato na matumizi (Tunategemea kupokea mihtasari hiyo hivi karibuni kama ilivyoagizwa)
·         Uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo Kilolo umefanywa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mh. Fakih  Jundu tarehe 30 April 2013 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010, Ibala ya 187. Jengo hili la kisasa la Mahakama hii limegharimu jumla ya Shilingi Milioni Mia mbili thelathini  laki moja thelathini  na saba elfu mia mbili themanini na senti arobaini  (Tsh. 230, 137,280.40/=).

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA JANUARI – APRIL 2013

Wilaya ya Kilolo Kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 iliidhinishiwa shillingi Bilioni sita arobaini na tatu milioni laki tatu themanini na mbili elfu, miambili sitini na tatu na senti kumi na tano(6,043,382,263.15/=) ikiwemo bakaa ya Shilingi Bilioni moja milioni mia moja   kumi na moja na thelathini na tisa elfu mia tano themanini na mbili na senti thelathini na tatu ( 1,111,039,582.33) ya mwaka 2011/2012 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.Hadi kufikia mwezi April 2013 Halmashauri ya Wilaya ya kilolo Imepokea Jumla ya Tshs. Bilioni nne  milioni mia moja thelathini na sita laki mbili  kumi na tatu elfu mia sita ishirini na nane na senti sitini  na tatu (4,136,213,628.63) ikijumuishwa na bakaa ya mwaka 2011/2012.Jumla ya   fedha zilizotumika  kwa kipindi cha Julai hadi April, 2013 ni Tshs. Bilioni mbili milioni  mia nne themanini na tisa laki  tatu na sita elfu  mia nne hamsini na moja  na senti tisini na tisa (2,489,306,451.99) Kwa ajili ya utekelezaji wa miradi  mbalimbali ya maendeleo.Hivyo inafanya Wilaya kuwa na bakaa ya Tshs. Bilioni moja milioni mia sita arobaini na sita laki  tisa na saba elfu mia moja sabini na sita na senti sitini na nne (1,646,907,176.64) za miradi ya Maendeleo. Aidha kwa kipindi cha Januari hadi April 2013 Wilaya imetekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo kama ilivyoanishwa kisekta hapa chini.

IDARA YA UJENZI

Jumla ya Tshs.Bilioni moja milioni mia saba na kumi  laki tano hamsini na moja elfu (1,710,551,000/=) zimetengwa katika utekelezaji wa shughuli za Ujenzi ikiwa hadi April,2013 imetumia jumla ya Tshs. Milioni mia nne na kumi laki  nane themanini elfu mia nne.(410,880,400/=) katika kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo :-Matengenezo ya kawaida (Routine Maintenance) kwa jumla ya Km.30 kama ifuatavyo;-
·         Matengenezo ya kawaida na kudumu barabara ya Ilula Mjini KM 7 na  Kazi inaendelea
·         Matengenezo ya kawaida na kudumu barabara ya Ihimbo - Kising'a KM 9  na Kazi ya kuweka kifusi imesimama kutokana  na  mvua zinazoendelea kunyesha.
·         Matengenezo ya kawaida barabara ya Kilolo - Ng'uruhe KM 7 na  Kazi inaendelea
·         Matengenezo ya kawaida barabara ya Kitowo - Mwatasi  KM 7.Kazi inaendelea.

Matengenezo ya sehemu korofi (Spot improvement) jumla ya  Km. 73 kwa mchanganuo ufuatao:- 
·         Matengenezo ya sehemu korofi barabara ya Kidabaga - Bomalang'ombe 9 KM, Ilula - Vitono - Uhambingeto KM 7,  Kilolo Mjini na  Kazi inaendelea.
·         Matengenezo ya sehemu korofi barabara ya Bomalang'ombe - Mwatasi KM 7, Ukumbi - Masege KM 5, Mawambala - Winome KM 6, Wotalisoli - Udekwa KM 15, Mwatasi -Ng'ingula KM 6 , Msonza - Kimala KM 8.  Kazi ya kuweka kifusi imesimama kutokana na  mvua zinazoendelea kunyesha
·         Matengenezo ya sehemu korofi barabara ya Ikuvala - Kipaduka - Ikuka KM 11 na kazi imekamilika

 Matengenezo ya Muda maalum (Periodic Maintenace) barabara ya Ilula - Ibumu KM 15 na barabara ya Makungu - Mlafu KM 6,

Aidha Wilaya inaendelea na ufunguzi wa barabara mpya za Idete - Kiwalamo - Kimala  KM 16 na Kazi ya ujenzi wa barabara hizi umesimama kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo hayo. Pia ufunguzi wa Barabara ya Ihimbo – Kitelewasi Km.20 unandelea kufanyika na Mkandarasi yupo eneo la kazi anaendelea na ujenzi huo.

Madaraja/makalvati na mifereji ya maji
·         Ujenzi wa daraja barabara ya Ukumbi - Pomerini (Concrete deck)kazi imekamilika
·         Ujenzi wa madaraja mawili na vivuko barabara ya Idete - Kiwalamo – Kimala.kazi imesimama kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
·         Ujenzi wa Mifereji ya mawe barabara ya Ilula - image ( Image no. 1),kazi inaendelea
·         Ujenzi wa Daraja la Kiwalamo 20m – 3 Span Kazi iko katika hatua ya manunuzi
Aidha Wilaya inaendelea na Ujenzi wa Nyumba  3 za watumishi Makao Makuu ya Wilaya na hatua iliyofikia ni ya Manunuzi.

Matengenezo haya yanafanywa kwa kutumia fedha zinazotokana na vyanzo mbalimbali baadhi ya vyanzo hivyo ni:-
  • Fedha kutoka mfuko wa barabara (Road Fund)
  • Fedha za Wadau/Wafadhili kutoka Food Aid Counter Part Fund  (FACTF) na New Forest Co. LTD
  • Fedha kutoka Ruzuku Maalum ya Maendeleo- Capital Development Grant (CDG)

 SEKTA YA MAJI

Katika kipindi cha mwezi Januari  2013 hadi April 2013, Sekta ya Maji imeendelea kutekekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa shughuli hizo zinatarajia kutumia Jumla ya Tshs. Milioni mia saba na nne laki moja thelathini na saba elfu (704,137,000/=) na tayari Tshs. Milion hamsini na nane laki  mbili thelathini na saba elfu( 58,237,000) zimeshatumika. Kwa mchanganuo ufuatao:-
·         Ujenzi wa mradi wa maji Ruahambuyuni ( hii ilikuwa ahadi ya Mhe. Waziri Mkuu alipotembelea Ruaha Mbuyuni na Tayari Tshs. Milioni ishirini (20,000,000/=) zimeshapokelewa). Kazi zilizopangwa ni pamoja na kujenga chujio,kujenga pump Machine pamoja na survey.Aidha Upimaji (Survey) ulifanyika kinachoendelea ni kazi ya usanifu
·         Ukarabati wa mtego wa maji wa Idunduge unaopeleka maji katika kijiji cha Iyai- Image.
·         Usimamizi wa uchimbaji visima vifupi na vya kati chini ya ufadhili wa MAUA projects (Maji, Usafi na Afya) katika Vijiji vya Lundamatwe kisima 1 na Isoliwaya Visima 3.
·          Ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Ikula na Vitono ambao muda wowote utaanza kutekelezwa kwa kuwa Wakandarasi wameshapatikana pamoja na idhini ya utekelezaji (no objection) toka Wizara ya Maji/Benki ya Dunia.
·         Kuimarisha mifumo ya maji katika Mamlaka za Maji katika Miji ya Ilula kwa upanuzi wa mradi  kwenda Mtua km.1.8,Madizini km2.3.Ukarabati line kuu ya Ilomba,vifaa vya ujenzi vimeshanunuliwa na kazi inaendelea kufanyika.
·         Kuimarisha mifumo ya maji katika Mamlaka za Maji katika Miji ya  Kilolo kwa Kupeleka maji Kitongoji cha Itunduma km 2,kujenga vituo viwili vya maji,ujenzi wa tank lita 5000 pamoja na ukarabati wa intake Na.2 ya maji (Mosongela).Kazi inaendelea kufanyika.
·          Aidha miradi ya maji ya Ruaha Mbuyuni na Mamlaka za maji za Ilula na Kilolo zinaendelea kufanyika.

SEKTA YA KILIMO,MIFUGO NA USHIRIKA

 Katika kipindi hiki  Sekta hii imefanya Shughuli mbalimbali zikiwemo Kuwezesha uchanjaji wa mbwa dhidi ya kichaa cha mbwa,Kufanya mikutano ya uhamasishaji kwa wakulima juu ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa katika vijiji  vya Idegenda na Mbawi,Kuwezesha uundaji wa vikundi viwili vya wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kwa vijiji vya Idegenda na Mbawi,Kutoa mafunzo kwa vikundi 2 vya Mbawi na Idegenda juu ya ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa Kuandaa na kuweka mabango ya kuutambulisha mradi katika vijiji hivyo na Kuwezesha ununuzi na usambazaji wa mbuzi wa maziwa katika vijiji vya Kimala, Mhanga na Idunda kwa Tshs.Milioni tisa, laki tano na ishirini na tatu elfu (9,523,000) kwa ufadhili wa Eastern Arc Mountains Conservation Endownment Fund (EAMCEF).

Kwa   upande wa Kitengo ya Ushirika ,shughuli zilizofanyika ni pamoja na Kufanya ukaguzi wa hesabu za SACCOS za NYAIM (Nyanzwa, Igunda na Mgowelo), Kilolo, Kitonga na kikundi cha wakusanya nyanya Ilula.Kufanya uhamasishaji wa uundaji wa SACCOS ya Image.Kutoa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa SACCOS ya NYAIM kwa viongozi wa bodi. Kufanya usajili wa SACCOS mpya ya Upendo iliyoanzishwa katika kijiji cha Kitowo kata ya Ukumbi na SACCOS Mpya ya Mpoki ambayo makao makuu yapo katika kata ya Ng’uruhe.
 Aidha mpaka sasa tumepokea kiasi cha Tshs.Milioni thelathini na nane  Laki tisa sabini na tano Mia saba thelathini na sita elfu (38,975,736/=) ikiwa ni kwa ajili ya  vikundi katika vijiji vya Isele, Masisiwe, Ng’ingula, Ng’ang’ange, Mdeke, Idasi, Mwatasi, Nyawegete na Luhindo kwa ajili ya kuwezesha uanzishaji wa vitalu vya miche ya chai.
 Bajeti  ya mwaka 2012/2013 ni Tsh.Milioni mia tatu sabini na tatu Laki nane tisini na moja elfu na thelathini na nne (373,891,034/=)  za Programu ya maendeleleo ya Kilimo Wilayani District Agriculture Development Plans  (DADPs).

SEKTA YA ELIMU SEKONDARI

 Katika kipindi cha Januari hadi Aprili Sekta ya sekondari imeweza kutekeleza shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na:-
·         Kugawa fedha za ruzuku katika shule  22 za sekondari ambazo ni Kilolo, Ilula, Dabaga, Kitowo, Lukani, Lulanzi, Lundamatwe, Madege, Masisiwe, Mawambala, Mazombe, Mlafu, Mtitu, Ngangwe, Uhambingeto, Udizungwa, Lukosi, Udekwa, Irole, Ukwega, Nyalumbu na Selebu.
·         Ujenzi wa madarasa mawili katika shule mbili  za lulanzi na Mawambala,
·         Ununuzi wa mobile laboratory 2 na kuzigawa katika shule mbili za kilolo  na kitowo,
·         Uendeshaji wa mtihani wa kidato cha sita katika shule tatu za Pomerin, Image na Ilula.
·         Ukamilishaji wa ujenzi wa  madarasa 3 kwa kila shule za  Sekondari za Madege,Mlafu,Mazombe,Mtitu,Lukosi na Kitowo.
·         Ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba za walimu katika shule za sekondari za Ngangwe, Lundamatwe, Kilolo, Makwema na Udekwa.

TAARIFA YA MFUKO WA ELIMU WA WILAYA (KETF)

·         Fedha zilizopo benki ni Tshs. Milioni tano laki saba arobaini na mbili  elfu mia nane tisini na nane (5,742,898.00) kama inavyoonesha kwenye bank statement.
·         Vifaa vilivyopo ni bati 270, bati 30 ziligawiwa katika sekondari ya Makwema kuezekea choo cha shule,aidha bati zilizobaki zitagawiwa katika shule za sekondari za Dabaga, Uhambingeto, Ukwega

Jumla ya Tshs.Milioni miamoja sitini na nane na thelathini na tisa elfu  mia sita na moja (168,039,601) zimeingizwa kwenye Akaunti za shule husika isipokuwa fedha za ruzuku.









USAJILI WA SHULE MPYA ZA SEKONDARI.

Usajili wa Shule mbili za sekondari  za Kata ambazo ni Shule ya Sekondari ya Ipeta iliyopo Kata ya Bomalang’ombe imepewa namba ya usajili S.4688   na shule ya Sekondari ya Luganga iliyopo Kata ya Nyalumbu imepewa namba ya Usajili ya S.4689.

Aidha shule ya Sekondari ya Udzungwa imepewa kibali cha kuongeza mikondo ya Kidato cha tano kwa barua yenye Kumb.Na.SPED/292/457/10/110 ya tarehe 14/02/2013 iliyotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Masomo yatakayofundishwa ni ya Mchepuo wa CBG  na HGL kwa wasichana tu.

MAPOKEZI YA WALIMU WAPYA.

Katika kipindi cha Januari hadi April 2013 Wilaya imepokea walimu wa shule za Msingi na Sekondari kwa mchanganuo ufuatao:-
·         Wilaya imepokea walimu 150 wa Idara ya Elimu Msingi ambao tayari wamesharipoti na kufikishwa kwenye vituo vya kazi.
·         Wilaya ilipangiwa walimu 82 wa shahada na walimu 42 wa stashahada.Walimu walioripoti na kupangiwa vituo vya kazi ni walimu 66 wa shahada na walimu 40 wa stashahada. Hivyo walimu 18 bado hawajaripoti.

SEKTA YA AFYA.

Sekta ya Afya imetekeleza shughuli za Kununua dawa na vifaa tiba ili kuongezea pale ambapo dawa toka MSD hazikutosha, Kufanya kikao cha pamoja na Waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma, Maafisa Afya na CHMT (Council Health Management Team). Kufanya usimamizi elekezi katika vituo 53 vya kutolea huduma za Afya wilayani.Ununuzi wa Solar power na ufungaji Katika Zahanati ya Kimala. Ujenzi wa shimo la kuchomea taka katika Kituo cha Afya Kidabaga( Placenta Pit).Kufanya usambazaji wa chanjo, dawa na vifaa tiba pamoja na  kulipa  gharama za mawasiliano (on call allowance) ikiwa jumla ya Tshs.Milioni tisini laki tatu na thelathini na saba elfu (90,337,000)   zimetumika kukamilisha kazi hizo. Aidha  fedha za Mfuko wa Pamoja wa Afya ( Health Basket  Fund), Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii(CHF)  na  Matumizi mengineyo(OC) zimetumika kufanikisha kazi hizi.
 Aidha Wilaya inaendelea na Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya awamu ya pili na  kwa sasa ujenzi upo  hatua ya Msingi.Ujenzi wa Chumba cha upasuaji Kidabaga HC (Awamu ya pili) ikiwa kwa sasa ipo hatua ya bimu,Ujenzi wa Zahanati mpya za Lugalo,Masege na Mbawi ikiwa kazi hizi zipo hatua ya manunuzi kupitia Mpango wa maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM) pamoja na fedha za Ruzuku Maalumu ya Maendeleo CDG(Capital Development Grant) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati hizo.Ukarabati wa zahanati ya Ifuwa ambayo imekamilika Jumla ya Tshs.Milioni miambili arobaini na tisa (249,000,000/=) zimetengwa kukamilisha kazi hizo.

SEKTA YA ARDHI, MALIASILI, MISITU NA MAZINGIRA
 Sekta ya Ardhi, Maliasili,Misitu na Mazingira  imeweza Kupima mashamba ya wananchi katika Kata ya Udekwa na Dabaga.Kutayarisha Database ya namba za nyumba kwa ajili kukusanya kodi za majengo katika Mji wa Ilula.Kulipa fidia ya ardhi na mali kwa wananchi waliotwaliwa ardhi zao kwa ajili ya uendelezaji wa Mji wa Kilolo ambapo kiasi cha Tshs Milioni ishirini na tisa (29,000,000/=) zilitolewa fidia kwa wananchi 29.Kuandaa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi wa Kijiji kimoja  cha Ifuwa.Kutambulisha mradi wa upandaji miti, ufugaji nyuki na kilimo cha uyoga katika vijiji 20 vya Nyanzwa, Mgowelo, Msosa, Mahenge, Irindi, Magana, Ikokoto. Ilambo, Ibumu, Iyai, Image na 8, Isagwa, Makungu, Luhindo, Lusinga, Ilamba, Ibofwe, Imalutwa, Mazombe na Lugalo.Kutoa mafunzo ya wajibu na majukumu kwa kamati za maliasili na upimaji wa mipaka misitu kwa Vijiji vya Masalali, Bomalangombe, Mkalanga, Nyanzwa na Mgowelo kwa jumla ya Tshs. Milioni sabini na nne laki nne thelathini na sita elfu mia nne na kumi (74,436,410/=) katika kukamilisha kazi hizo.

FEDHA ZA RUZUKU MAALUM YA MAENDELEO (CDG) KWENDA NGAZI ZA VIJIJI

Katika kipindi cha Januari hadi April, 2013, Miradi iliyowezeshwa kupitia fedha za Ruzuku Maalum ya Maendeleo ni pamoja na:-
·   Ukamilishaji  wa madarasa,vyoo na nyumba za walimu kwa shule za Msingi 34
·   Ukamilishaji wa majengo kwa sekondari za Ipeta,Ibumu,Ilula mwaya (Luganga sekondari),Ngagwe,Selebu,Irole,Kimala,Mhanga,Igunda,Dabaga na Mawambala;
·   Ukamilishaji wa Wodi ya Akina mama Ikula,Ukamilishaji wa zahanati ya Mbawi;
·   Ukamilishaji wa ofisi ya Kijiji cha Lugalo,Itungi,Ng’ang’ange  na Ofisi ya kata Lugalo
Jumla ya Tshs.121, 000,000/= zimeingizwa kwenye akaunti za Taasisi husika kama vijiji na shule na utekelezaji upo hatua mbalimbali.

MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO JIMBO LA KILOLO (CDCF)
Jumla ya Tshs 52,659,814/= zimepokelewa katika kipindi cha Januari hadi April, 2013 kwa ajili ya kuendeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika Jimbo la Kilolo ikiwemo kuchangia maeneo ambayo tayari wananchi wameshachangia nguvu kazi.
·         Ukarabati/ukamilishaji wa ujenzi wa majengo kwa Shule za Msingi 15 ambazo ni Luhindo, Luganga, Ikuvala, Mwaya, Uhambingeto, Iwungi, Mtakuja, Ikokoto, Ibumu mkondo B, Isagwa, Wangama, Mdeke, Ndengisivili na Masalali.
·         Kuwezesha ujenzi wa  mabweni Sekondari za Mlafu na Mawambala,
·         Kuwezesha Ujenzi wa Wodi la Akina mama zahanati ya Ikula,
·         Kufunga umeme wa jua (solar Power) zahanati ya Lukani
·         Ukamilishaji wa  ujenzi wa madarasa Sekondari za Ibumu na Ipeta.

Aidha Jumla ya Tshs.Milioni ishirini na tatu na laki tano (23,500,000/=) ziliidhinishwa na Kamati ya Mfuko wa Jimbo iliyokaa tarehe 05/03/2013 na fedha ziliingizwa kwenye akaunti za Taasisi husika.Mgao wa awamu ya Pili unatarajia kufanyika Mwanzoni mwa mwezi Mei, 2013.

 

Changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha Januari hadi April, 2013.

 Wilaya ya Kilolo ilikabiliwa na changamoto zifuatazo:

  1. Fedha zilizoidhinishwa kutofika kwa wakati au kufika pungufu.

  1. Bajeti ndogo hasa juu ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara hali inayopelekea baadhi ya maeneo ya barabara za Idete – Itonya km 8, Msonza – Kimala km 7, Kimala – Idunda – Mhanga km 10, Mhanga – Itonya – Uluti km 16, Ng’ingula – Madege km 5, Ng’ingula – Masisiwe km 10, Kimala – Ukwega km 12, Makungu – Mlafu km 6, Ikokoto A – Ikokoto B km 6.5, Wotalisoli – Udekwa km18 na Ukumbi – Mawambala km 17 kutopitika hasa katika kipindi cha mvua.

      iii.            Uchangiaji hafifu wa Wananchi katika utekelezaji miradi ya maendeleo kama ambavyo maelekezo  ya kisera yanavyosema,hali hii imepelekea kuwa na ugumu na uchelewashaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
    iv.            Kutopata Watumishi wapya (Ajira Mpya) walioko kwenye Mpango na bajeti 2011/12 isipokuwa walimu wa Idaraya ya Elimu  Msingi na Sekondari tu.
      v.            Vikwazo juu ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya wilaya katika vipengele viwili kama ifuatavyo;
a)     Kutokuwepo kwa viwango vya leseni za biashara toka Wizara ya TAMISEMI, Viwanda na Biashara.
b)    Ushuru utokanao na chanzo cha Stendi ya Ilula, Magari kutoingia stendi na kulipa ushuru.
c)    Ukosefu wa fedha za kulipia fidia za viwanja kwa wakati.


………………..
GERALD GUNINITA
MKUU WA WILAYA
KILOLO






0 comments:

Post a Comment