Main Menu

Wednesday, November 28, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA SHULE YA MSINGI YA KILOMO-MJINI BAGAMOYO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Sam Elangalloor, wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria uzinduzi wa Shule ya Msingi Kiromo, iliyopo Wilaya ya Bagamoyo-Mkoa wa Pwani, iliyokarabatiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika Nov 27, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania,Sam Elangalloor, wakati akionyeshwa vitabu vilivyotolewa na Kampuni hiyo kwa Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shule hiyo baada ya kukamilika kwa ukarabati.Nov 27, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) wakati akionyeshwa Madawati yaliyotolewa na Kampuni hiyo kwa Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Shule hiyo baada ya kukamilika kwa ukarabati.Nov 27, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Mh. Shukuru Kawambwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za Mkononi, Sam Elangalloor, kukagua maeneo ya Shule ya Msingi Kiromo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo, uliofanyika Nov 27, 2012, shuleni hapo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliofanywa na kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sam Elangalloor, kuhusu matumizi na makusudio ya mafunzo ya Kompyuta wakati alipotembelea katika chumba cha Kompyuta, baada ya kuzindua rasmi shule ya Msingi, Kiromo, Nov 27, 2012.

0 comments:

Post a Comment