Pamoja na baadhi ya wananchi kulalamikia uchaguzi wa wawakilishi wa mabaraza ya Katiba, Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji mstaafu Joseph Warioba amesema hawako tayari kurudia uchaguzi huo.
Katika kikao chake na waandishi wa habari jijini Dar es salaa leo, Warioba amesema kama kuna watu wamepatika kwa njia ya mizengwe na rushwa wao hawana jukumu la kuwashitaki kwani wenye jukumu hilo ni taasisi yakuzuia na kupambana na rushwa nchini
TAKUKURU.
Warioba Amekiri kuwepo kwa taarifa hizo ikiwemo changamoto ya wananchi kutoridhika na taratibu za uchaguzi zilivyofanyika bila kuzingatia mwongozo wa tume na kuongeza kuwa wanachofanya wao ni kuhakikisha kuwa wanasimamia sheria ya mabadiliko ya katiba.
Aidha amesema tume itafanya maamuzi magumu katika kuandaa rasimu ya katiba ambayo inatarajiwa kuwa tayari katikati ya mwezi wa sita mwaka huu na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa, jumuiya na taasisi nyingine kuwaachia wananchi watoe maoni yao badala ya kuwaingilia.
Akizungumzia haki ya watu wenye ulemavu kupata nafasi ya kushiriki katika mabaraza ya katiba Warioba amesema tume itashirikiana na shirikisho la watu wenye ulemavu na kupata wawakilishi wanne kwa kila chama cha walemavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment