Main Menu

Sunday, July 7, 2013

BOLIVIA YALIPIZA KISASI KWA NCHI ZA ULAYA KWA KUMPA HIFADHI SNOWDEN

Viongozi wa nchi tatu za Amerika ya Latini wamesema wako tayari kumpa hifadhi mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani NSA Edward Snowden ambaye amefichua taarifa kuhusu mradi mkubwa wa ujasusi wa Marekani kote duniani.  


Bolivia imejiunga na Venezuela na Nicaragua ambazo zimesema ziko tayari kuma hifadhi Snowden. 


Rais Evo Morales wa Bolivia amesema atampa hifadhi Snowden kama njia ya kulalamikia hatua ya nchi za Ulaya ya kuizuia ndege yake iliyokuta ikitoka Moscow kwa madai kuwa ilikuwa imembeba Snowden. 


Morales amesema nchi za Ulaya ziliizuia ndege yake kwa amri ya Marekani. 


Snowden, hivi karibuni alifichua kwamba Marekani imekuwa ikidukua mitandao ya intaneti na kukusanya taarifa za siri za watu kote duniani; jambo ambalo ni kinyume na sheria za kimataifa.


 Snowden pia alifichua kwamba mashirika ya kijasusi ya Marekani ya CIA na NSA yamekuwa yakinasa mazungumzo ya simu kote duniani. 


Aidha alifichua kuwa Marekani imekuwa ikiwafanyia ujasusi maafisa wa kidiplomasia wa nchi za Umoja wa Ulaya jambo ambalo limeibua hasira kote Ulaya.  


Snowden hivi sasa amepata hifadhi ya muda katika uwanja wa ndege Moscow jambo ambalo limepelekea kuzorota uhusiano wa Marekani na Russia.

0 comments:

Post a Comment