Main Menu

Sunday, July 7, 2013

WAISLAMU WAKUMBUSHWA KUSAIDIANA KIPINDI CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein amesema kuwa ni dhima ya Waislamu kutilia mkazo suala la kuishi pamoja kama ndugu katika misingi ya kuheshimiana, kustahamiliana na kupendana, kama Uislamu unavyofundisha. 

Amesema kuna kila sababu kwa Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema anazowapa kila uchao.


Sambamba na hayo, Dk Shein amewakumbusha Waislamu kuswali na kuwa na njia bora za kutumia mali walizojaliwa na Mungu na kuzidi kukumbushana na kuhimizana kutoa zaka na sadaka. 


Rais wa Zanzibar amewataka Waislamu kutayarisha nafsi zao kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambao husogeza pepo karibu zaidi na waja wa Mwenyezi Mungu. 


Dkt Shein amewahimiza Waislamu kujiepusha na Israfu wakati wa Ramadhani na pia kuwataka wanabiashara kutoongeza kiholela bei ya bidhaa muhimu wakati wa mfungo.

0 comments:

Post a Comment