Main Menu

Tuesday, October 29, 2013

TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA POOL YAFANYA KWELI KWENYE MASHINDANO YA AFRIKA NCHINI MALAWI


Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4.
Mgeni rasmi,Mjumbe wa Baraza la Michezo Nchini Malawi, Sharaf Pinto(wa pili kushoto) akiwa na mabingwa wa Singles(mchezaji mmoja mmoja).Kutoka kulia ni mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na Bingwa gwa Afrika kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwakabidhi medali zao Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Mabingwa wa Afrika wa mchezo wa pool wakiwa katika picha ya pamoja.Kutoka kushoto ni Bingwa wa Afrika kutoka Tnzania, Patrick Nyangusi,mshindi wa pili kutoka Afrika Kusini, Vishen Jagdev na mshindi wa tatu kutoka Zambia, Moses Mofya mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao .

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika .
Bingwa wa Afrika wa Safari Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akiwa katika picha ya pamoja na warembo wa Blantyre Malawi mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya medali ya zahabu mwishoni mwa wiki.

MCHEZAJI wa timu ya Safari Pool Taifa, Patrick Nyangusi ameibuka Bingwa wa Afrika katika mashindano ya mchezaji mmoja mmoja(singles) wanaume yaliyojumuisha timu saba kutoka katika Nchi sita za Afrika.

Patrick Nyangusi aliupata ubingwa huo kwa kumfunga mchezaji bora wa Afrika Kusini, Vishen Jagdev 6-4,katika mchezo ambao ulisisimua wapenzi na mashabiki wengi wa mchezo huo uliofanyika katika ukumbi wa kisasa wa Roben Complex jijini Blantyre.

Nyangusi kwa ubingwa huo alizawadiwa medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili alichukua mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini ambaye alizawadiwa Medali ya Silver wakati  mshindi wa tatu ni Moses Mofya kutoka Zambia ambaye alimfunga mchezaji wa Tanzania, Omary Akida, 5-3 na hivyo Moses Mofya kuzawadiwa Medali ya Fedha na nafasi ya nne ilichukuliwa na mchezaji kutoka Tanzania, Omary Akida.

Upande wa timu zilizowakilisha Nchi, Zambia waliibuka mabingwa katika mchezo ambao uliendeshwa kwa mfumo wa ligi ambapo Zambia waliongoza kwa pointi 14.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na timu kutoka Nchi ya Afrika Kusini kwa pointi 12,na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Nchi ya Tanzania ambao walipata pointi 9, wakati nafasi ya nne ilibaki kwa wenyeji Malawi ambao walipata pointi 4.

Akizungumza Mkurugenzi wa mashindano ya AAPA (All Africa Pool Associations), Rick Schoenlank, alizipongeza Nchi zote zilizoshiriki mashindano hayo,pili aliwapongeza waandaaji wa mashindano kwa maandalizi mazuri na mwisho aliipongeza Tanzania kwa kutoa bingwa wa Singles kwa mwaka 2013.

Nae mgeni rasmi aliyefunga mashinndano hayo, Mjumbe wa Baraza la Michezo la Nchini Malawi, Sharaf Pinto, kwa niaba ya Waziri wa michezo wa Malawi,aliipongeza pia Tanzania kwa kutoa bingwa Singles na kuwaomba Tanzania kuwa karibu na wachezaji wa Malawi ili kubadilishana uzoefu na udugu pia kwa kutembeleana na kucheza mechi za kirafiki.

Lakini pia aliwapongeza Zambia kwa kutwaa ubingwa wa timu na vilevile aliwapongeza Malawi kwa nafasi waliyopata si mbaya sana, ni nafasi ambayo inawafanya wajiandae vyema kwa mashindano yajayo.

Mwisho aliwapongeza kila Nchi kwa kuleta uwakilishi na kuwatakia safari njema ya kurejea Nchini salama mpaka mashindano mengine mwakani.

Mashindano ya mwaka huu yalijumuisha Nchi takribani 6, ambazo ni Afrika Kusini, Zambia,Tanzania,Lesotho,Namibia na wenyeji Malawi 1 na Malawi 2.

Timu ya Safari Pool ililiyokwenda Malawi ina jumla ya wachezaji 8, ambao ni Mohamed Idd, Patrick Nyangusi Festo Yohana ,Mereczedec Amadeus,Omary Akida,Abdalah Hussen ,Godfrey Swain a Nahodha Charles Vernas na viongozi watatu ambao ni Meneja wa timu Nabil Hiza,Katibu wa chama cha pool Taifa, Amos Kafwinga na Makamu Mwenyekiti, Fred Mush

Mashindano ya AAPA mwakani yanatarajiwa kufanyika Tanzania jijini Dar es Saalaam.

0 comments:

Post a Comment