Main Menu

Monday, July 20, 2015

MATHEW FLAMINI KUIKACHA ARSENAL



Kiungo wa klabu ya Arsenal Mathew Flamini amekubali kujiunga na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31alijiunga na klabu ya Arsenal akitokea klabu ya AC Milan ya nchini Italia mwaka 2013 na amekuwa na wakati mgumu wa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha Arsenal.

Flamini ameanza katika michezo 15 tu ya Ligi Kuu akiwa na Arsenal msimu uliopita kutokana na uwezo mzuri aliounesha kiungo Francis Coquelin namkataba wake unaisha mwaka 2016.

Tayari klabu ya Galatasaray imemsajili mshambuliaji Lukas Podolski kutoka Arsenal.

0 comments:

Post a Comment