Takriban watu 35 wameuawa katika
ajali ya barabarani karibu na mji wa Mwingi Mashariki mwa Kenya.
Duru za polisi zilisema kuwa wengi
wa waliofariki walikuwa wanafanya kazi mjini Nairobi, na walikuwa wanarejea makwao
kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Jumatatu.
Farah Aden Ali, aliyenusurika kifo alisema
kuwa basi hilo lilikuwa limejaa watu kupindukia na lilianguka baada ya dereva
kupoteza mwelekeo.
Barabara nyingi nchini Kenya ziko
katika hali mbaya na vile vile hali ya mabasi mengi ni mbaya.
Afisaa wa trafiki Samuel Kimaru
alisema kuwa takriban abiria 35 walifariki na wengine 50 kujeruhiwa katika
ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Bwana Aden Ali aliambia BBC kuwa
vikundi vya uokozi viliwasili katika eneo la ajali masaa manne baada ya ajali
kutokea hali iliyosababisha waliokuwa wamekwama ndani ya basi hilo kufariki.
Basi lilikuwa limejaa watu na
lilikuwa linaelekea katika miji ya Mandera na Garisa
Ali alisema kuwa dereva alikuwa na
matatatizo na gia ya basi hilo tangu kundoka Nairobi
Alisema alikuwa amelala lakini
aliamka muda mfupi baada ya ajali kutokea.
''Dereva alipoteza mwelekeo. Alikua
anajaribu kulirejesha basi barabarani , lakini likaanguka kwa upande,'' alisema
Ali.
Babaraba za Kenya huwa na msongamano
mkubwa wa magari hususan kabla ya uchaguzi mkuu huku wafanyakazi wa miji
wakielekea mashinani kupiga kura.
CHANZO BBCSWAHILI
0 comments:
Post a Comment