Papa Benedikto wa 16 amejiuzulu rasmi leo kama kiongozi
wa kanisa katoliki ulimwenguni.
Katika hotobu yake ya
mwisho kwa umati wa watu zaidi ya laki moja na nusu
waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro jana,
Benedikto wa 16 ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani, aligusia
changamoto zilizolikumba kanisa wakati akiwa kiongozi
wake, na kusema kuwa kuna wakati ilionekana kwake kama
mungu amesinzia.
Hata hivyo, aliongeza kuwa mara zote alifahamu kuwa
Mungu ndiye nahodha wa meli ya kanisa katoliki, na
kwamba kamwe asingeiacha meli hiyo izame.
Kesho Ijumaa makardinali wataanza mchakato wa
kumchagua papa mpya. Benedikti wa 16 atajulikana sasa
kama Papa Emeritus, na atahamia katika chumba cha
kitawa mjini Vatikani mwezi Aprili.
0 comments:
Post a Comment