Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi
jijini Dar es salaam, kesho jumanne itaingia katika siku ya nne kwa
kuwakutanisha Azam FC
dhidi ya Malakia kutoka Sudani Kusini, mchezo utakochezwa katika uwanja wa
Taifa majira ya saa 10 kamili jioni.
Mchezo wa kwanza utakaoanza majira ya saa 8 kamili mchana
uwanja wa Taifa utazikutanisha timu za Al Shandy ya Sudan dhidi ya LLB ya
Burundi, huku uwanja wa Karume majira ya saa 10 kamili jioni Heegan FC ya
Somalia wataonyeshana ubavu dhidi ya APR kutoka Rwanda.
Jumatano kutakua na michezo mitatu ambapo mchezo wa
kwanza uwanja wa Taifa utawakutanisha Khartoum ya Sudan dhidi ya KMKM ya
Zanzibar saa 8 mchana, huku uwanja wa Karume saa 10 jioni KCCA ya Uganda
watawakaribisha Adama City kutoka Ethiopia.
Katika uwanja wa Taifa jumatano saa 10 jioni, Telecom ya
Djibout watakua wenyeji wa Yanga SC ambayo kocha wake mkuu Hans Van Der Pluijm
ameahidi kupata ushindi katika mchezo huo.
Hans amesema mchezo wa ufunguzi dhidi ya Gor Mahia
walipoteza kutokana na kucheza pungufu kwa takribani dakika 60, hivyo anawaanda
vijana wake kufanya vizuri siku ya jumatano na kuwapa furaha wanachama na
wapenzi wa Yanga SC.
0 comments:
Post a Comment