Main Menu

Wednesday, June 19, 2013

KILI MUSIC TOUR 2013 KUANZA KUKINUKISHA DODOMA JUMAMOSI JUNI 22


Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) chini ya Bia yake ya Kilimanjaro, inataraji kuanza rasmi tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama ‘Kili Music Tour’ wikiendi hii katika mji wa Dodoma.

Tamasha hii kubwa linatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi ya tarehe 22 Juni, 2013 mjini Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri na litajumuisha wasaniii 8 ambao ni Ally Kiba, Ommy Dimpoz, Professor J, Ben Pol, Lady Jay Dee, Lynex, Roma na Kala Jeremiah.

Mwaka huu Bia ya Kilimanjaro imebadilisha utaratibu wa tamasha hili la muziki ambalo lilikuwa linajulikana kama KTMA Winners Tour na lilikuwa likijumuisha wasanii walioshinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards pekee.

Mwaka huu bia ya Kilimanjaro imebadilisha jina la tamasha kuwa Kili Music Tour na litashirikisha wasanii wote kwa ujumla na sio washindi wa tuzo za KTMA pekee.

“Kili Music Tour imepanua wigo wake kwa kushirikisha wasanii walioshinda tuzo, wasanii waliokuwa kwenye mapendekezo ya tuzo na wasanii ambao hawakushiriki kabisa kwenye tuzo lakini wako juu kwenye tasnia ya muziki nchini. 

Hii ni kwenye kuhakikisha kuwa mashabiki wa muziki wanapelekewa wasanii wanaowapenda kwenye mikoa yako bila kubagua. Mwaka huu matamasha yameongezeka kutoka sita mwaka jana na kuwa nane.

Kili inaelewa ni jinsi gani watanzania wanajivunia mambo ya kitanzania kama muziki wetu wa bongo flava, dansi yetu ya kiduku, kandanda letu lenye ushabiki wa simba na yanga, lugha yetu ya kipekee na bia yetu ya Kilimanjaro inayowapa bonge la kiburudisho .

Ndio maana tumeongeza wigo wa Tamasha kama ishara ya shukurani kwa jinsi watanzania wanavyojivunia mambo ya kikwetu kwetu.” Alisema Bwana George Kavishe Meneja wa bia ya Kilimanjaro.

Msanii aliyebobea wa bongo flava ajulikanaye kama Kala Jeremiah naye alisema “ mwaka huu mashabiki wategemee kupata vionjo ambavyo hawajawai kuviona kwani mimi na wasanii wenzangu tumejipanga kikamilifu kuhakikish kuwa hatuwaangushi mashabiki wetu na kuwa tunawapa bonge la kiburudisho!” 

0 comments:

Post a Comment