Main Menu

Thursday, June 13, 2013

PAPA FRANSIS AKIRI KUSHINDWA KUDHIBITI VITENDO VYA USHOGA NA UFISADI KATIKA KANISA KATOLIKI

Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amekiri kushindwa kupambana na vitendo vya ufisadi na lobi ya watu wanaopenda kufanya ngono ya jinsia moja vilivyoshamiri huko Vatican. 

Akizungumza na wajumbe wa Mashirikisho ya Kidini ya Amerika ya Latini, Papa Francis amesisitiza kuwa, ndani ya Vatican kuna ufisadi mkubwa pamoja na lobi ya watu wanaofanya ngono ya jinsia moja. 

Ameongeza kuwa, kwa miongo kadhaa sasa Kanisa Katoliki limekumbwa na migogoro mikubwa ya ufisadi , utumiwaji  mbaya wa mali za kanisa, kuporomoka maadili na hasa suala la ubakaji watoto wanaopata mafunzo kwenye makanisa ya madhehebu hiyo katika nchi mbalimbali na hasa Marekani na Ulaya. 

Papa Francis amekiri kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo, na hivyo ameamua kulikabidhi kwa kamati ya makadinali wenye kuaminika, ili waweze  kulishughulikia.

0 comments:

Post a Comment