Main Menu

Thursday, June 13, 2013

LIONEL MESSI ATUHUMIWA KUKWEPA KULIPA KODI

Mwanasoka mahiri Lionel Messe anatuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi.

Messi pamoja na baba yake wanashutumiwa na waendesha mashitaka mjini Catalonia nchini Uhispania kwa kukwepa kulipa kodi kwa ofisi ya kodi  katika eneo hilo ya kiasi ya euro milioni 4 kati ya mwaka 2007 na 2009 kutokana na mapato ya ziada mchezaji huyo alipokea kutokana na kushiriki katika kuonekana  katika  mauzo ya kibiashara.

Messi mwenye umri wa miaka 25 ndiye mwanasoka aliyeifungia Barcelona mabao mengi zaidi katika historia ya kilabu hiyo na ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa shirikisho la soka duniani Fifa kwa miaka minne mfululizo.

0 comments:

Post a Comment