Main Menu

Sunday, August 4, 2013

WATU WASIOJULIKANA WAMEVUNJA TRANSIFOMA NA KUIBA MAFUTA NA NYAYA ZA KOPA

Watu  wasiojulikana wamevunja transfoma ya umeme na kuiba mafuta na waya za kopa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milion 70 katika mradi wa kusambaza umeme unaofanywa na kampuni ya Symbion  katika  kata ya Tubuyu na Tungi katika manispaa ya Morogoro .

Mwakilishi wa kampuni ya Symbioni akizungumza katika tukio hilo amesema hiyo sio mara ya kwanza kutokea na kuwa vitendo vya kuhujumu miundombinu ya umeme inakwamisha kukamilika kwa shughuli za kusambaza umeme kwa wananchi na kutaka jeshi la polisi kusaidia ili kupatikana kwa waliohusika .


Nao wananchi katika eneo la tubuyu wamelalamikia kitendo hicho huku wakitupia lawama huenda hujuma hiyo imefanywa na wataalamu wenye ujuzi na fani ya umeme huku wakiomba msaada wa vyombo vya sheria kuweza kuwatia hatia waliohusika kwani hujuma hizo zinasababisha kusimama  kwa mradi wa kusambaza umeme kwa wananchi.
NA ITV

0 comments:

Post a Comment