Main Menu

Tuesday, June 18, 2013

MKUTANO WA KILELE WA G8 WAMALIZIKA IRELAND YA KASKAZINI

Viongozi katika mkutano wa kilele wa mataifa nane yaliyoendelea kiviwanda uliyofanyika Ireland ya Kaskazini, wamekubaliana juu ya hatua mpya za kuwabana watu wanaosafirisha fedha kwa njia za haramu, wale wanaokwepa kodi kinyume na sheria na makampuni yasiyolipa kodi zinazostahili. 

Lakini mkutano huo uligubikwa na mgogoro wa Syria. 

Viongozi wa G8, akiwemo rais wa Urusi, Vladmir Putin, mshirika wa rais wa Syria Bashar al-Assad, waliunga mkono miito ya kufanya mazungumzo mjini Geneva haraka iwezekanavyo

. Mwenyeji wa Mkutano huo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, alisema viongozi hao kwa pamoja wanalaani matumizi ya silaha za kemikali na upande wowote, na kutaka kuruhusiwa wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wabaini ukweli kuhusiana na silaha hizo. 

Katika mkutano huo, viongozi walizindzua majadiliano ya biashara huru kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya.

0 comments:

Post a Comment