Nchini Kenya Muungano wa Walimu wa shule za Sekondarina Vyuo KUPPET
umetangaza kusitisha mgomo kwa muda ili kuruhusu mazungumzo na serikali.
Maafisa wa Kuppet wamewataka wanachama wao warejee darasani siku ya LEO ili muungano huo ufanye mazungumzo na serikali kama mahakama
ilivyo amuru.
Hatahivyo CHAMA cha Kitaifa cha Walimu (KNUT) kinasisitiza
kuwa mgomo unaendelea.
Katibu Mkuu wa Kuppet Akelo Misori amesema Bodi ya Magavana cha chama hicho wamekutana Jumanne na kuamua kusitisha mgomo.
Mgomo wa walimu Kenya ulianza Juni 25, 2013 ambapo ilitazamiwa
utaendelea hadi wakati ule serikali itakapowalipa walimu nyongeza ya
marupurupu ambayo yaliafikiwa 1997, miaka 16 iliyopita.
Mahakama Kuu nchini Kenya Jumatatu iliwaamuru walimu wote wanaogoma
warejee kazini Jumanne na kumtaka Waziri wa Leba Kazungu Kambi aunde
kamati ya kushauriana na vyama vya walimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment