Wednesday, June 10, 2015
USAJILI ULAYA WAENDELEA NA TETESI ZAKE
Tumalizie na taarifa za usajili ambazo zinasema kuwa klabu ya Manchster United ipo katika mchakato wa kumpata mshambulaiji wa klabu ya Atletico Madrid Mario Mandzukic.
Mshmabuliaji huyo amekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone hasa mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Hispania.
Tukibakia hapohapo katika klabu ya Manchester United,klabu ya PSG ipo tayari kuipa Manchster United beki wake wa kulia Gregory Van Der Wiel.
Ujio wa Gregory Van Der Wiel umetokana na klabu ya Manchester United kumkosa beki wa kulia wa Barcelona Dani Alves.
Dani Alves ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kukipiga kunako klabu ya Barcelona.
Naye kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa yupo tayari kutoa kiasi cha euro milioni 40 kuweza kupata saini ya mshambuliaji wa klabu ya Porto ya Ureno Yacini Brahimi.
Brahimi amekuwa na msimu mzuri sana na klabu ya Porto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment