Katika mchezo huo, timu ya Golden State Warriors
imefanikiwa kuchukua taji la NBA baada ya kuifunga timu ya Cleveland Cavaliers
kwa pointi 107 kwa 95 na hivyo kushinda kwa michezo 4-2.
Kwa ushindi huo Golden State Warriors imefanikiwa
kuchukua taji la NBA kwa mara ya nne katika historia ya timu hiyo ambapo imewachukua
miaka 40 tangu walipotwa ubingwa mara ya mwisho mwaka 1975.
Katika mchezo huo wachezaji wa Golden State Warriors
Andre Iguodala na Stephen Curry walifunga pointi 25 kila mmoja huku Lebron
James akifunga pointi 32 peke yake kwa upande wa Cleveland Cavaliers.
Mchezaji wa Warriors Andre Iguodala amechaguliwa kuwa
mchezaji bora wa mashindano.
0 comments:
Post a Comment