Wakati wachezaji wa vilabu mbalimbali wakivihama vilabu
vyao bila timu husika kunufaika kutokana na kumalizika kwa mikataba , hali hiyo
imetajwa kusababishwa na ukata wa timu za ligi kuu.
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa timu ya Ndanda Fc
Athumani Kambi ameiuambia mtandau huu kwamba timu hiyo haina mchezaji hata
mmoja mwenye mkataba baada ta ligi kumalizika.
Kambi amesema hali hiyo imechangiwa na timu hiyo kutokua
na fedha hivyo iliwapa wachezaji wake mkataba wa mwaka mmoja na baada ya ligi
kumalizika wanaanza upya kusajili.
‘’Hatuwezi kuwapa mikataba ya muda mrefu kwa sababu
hatuna hela na ni kwamba mpaka hivi sasa kuna wachezaji wanatudai mishahara yao’’
Alisema Kambi.
Ndanda iliyopanda ligi kuu msimu uliopita ilinusurika
kurudi daraja la kwanza baada ya kufanikiwa kupata ushindi katika mchezo wake
wa mwisho dhidi ya Yanga mjini Mtwara.
Ndanda Fc mbali ya kupata fedha za wadhamini wa ligi kuu Vodacom
na matangazo ya televisheni pia walipata milioni 50 kutoka kwa kampuni ya Binslum
Tyre Co. Ltd kwa ajilinya kutangaza bidhaa yake ya V Rabe.
Timu hiyo hivi sasa inapitia ripoti ya mwalimu wake Meja Mingange
na Ngawina Ngawina kwa ajili ya kufanyia maboresho kikosi hicho kwa ajili ya
msimu ujao.
Hata hivyo majaliwa ya kuendelea kuwa na kocha Mingange bado
ni hafifu baada ya kocha huyo kudaiwa kuikimbia timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment