Klabu ya PSG ipo tayari kutoa kiasi cha euro milioni 125
kwa ajili ya kupata saini ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano
Ronaldo.
Hali ya klabu ya Real Madrid kwa sasa si shwari kutokana
na timu hiyo kufanya vibaya msimu huu na hakuna matumaini ya benchi la ufundi
la timu hiyo chini ya kocha Carlo Ancelooti kuwepo tena msimu ujao.
Cristiano Ronaldo amevunja rekodi nyingi msimu huu
ikiwepo ya kuwa mfungaji bora wa pili wa klabu ya Real Madrid kwa kufikisha
idadi ya magoli 310.
Rekodi hiyo imemfanya Ronaldo kubakisha magoli 13 tu kuwa
mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid.
Kwa sasa nyota huyo anaongoza kwa ufungaji wa magoli
katika Ligi Kuu ya soka nchini Hispania akiwa na magoli 45 huku mpinzani wake
Messi akiwa na magoli 41.
0 comments:
Post a Comment