KLABU ya Real Madrid imemfukuza kocha Carlo Ancelotti baada ya kumaliza msimu bila ya kombe hata moja na ikiwa ni mwaka mmoja na siku moja tangu aipe timu hiyo taji la 10 la Ulaya.
Rais
wa klabu, Florentino Perez amethibitisha mbele ya Waandishi wa
Habari jana usiku juu ya uamuzi wa kumtimua kocha huyo wa tisa
katika miaka yake 12 ya kuwa madarakani, Lakini akazuiwa kwa muda
kumtaja Rafa Benitez kuwa kocha mpya.
Kocha
huyo wa zamani wa Liverpool anabaki kuwa mwenye nafasi kubwa ya kurithi
mikoba ya Ancelotti ambaye kufukuzwa kwake hakujawafurahisha wahezaji
na mashabiki.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ametangaza kumfukuza Ancelotti
Kutokana na rekodi ya rais wa klabu hiyo ya jiji la Madrid ilikua ni vigumu kwa kocha huyo kuendelea kubaki Real japo alikua anaungwa mkono wa wachezaji wengi akiwemo nyota wa timu hiyo Christian Ronaldo.
MAKOCHA TISA ALIOFUKUZA FLORENTINO PEREZ NDANI YA MIAKA 12
Vicente del Bosque (Juni 23, 2003)
Carlos Queiroz (Mei 24, 2004)
Jose Antonio Camacho (Septemba 20, 2004)
Marino Garia Remon (Desemba 30, 2004)
Vanderlei Luxemburgo (Desemba 4, 2005)
Fabio Capello (Juni 28, 2007)
Bernd Schuster (Desemba 9, 2008)
Manuel Pellegrini (Mei 26, 2010)
Carlo Ancelotti (Mei 25, 2014)
0 comments:
Post a Comment