Katika kuboresha kikosi na benchi la ufundi la timu
iliyopanda ligi kuu msimu ujao African Sports, uongozi wa timu hiyo upo katika
mipango ya kumuajiri kocha wa Mgambo Shooting Bakari Shime.
Meneja wa kocha huyo ajulikanae kama mchawi mweusi Martin
Kibua amesema tayari wameshapata ofa mbalimbali ikiwemo ya timu yake ya sasa ya
mgambo na timu ya African Sports.
Mkataba wa Shime na mgambo shooting unamalizika mwishoni
mwa mwezi huu.
Kuhusu mustakabali wa wapi atafanya kazi msimu ujao shime
amesema hiyo ni kazi ya wakala na meneja wake yeye kazi yake ni kufundisha
mpira tu.
Aidha Shime amesisitiza yupo tayari kufundisha timu
yoyote pasipo kujalisha ni ya taasisi au wanachama kwa sabuba ili ufanikiwe ni
lazima uzishinde changamoto.
African Sports ni miongoni mwa timu 4 zilizopanda ligi
kuu kwa ajili ya msimu ujao baada ya kuwa nje ya ligi kuu kwa miaka 23.
0 comments:
Post a Comment