Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Oliver Giroud ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi kuu ya
soka nchini England.
Mshambuliaji Olivier Giroud amekuwa katika kiwango
bora sana msimu huu kwani katika michezo minne
iliyopita ya Ligi kuu,Giroud ameifungia timu yake magoli matano na hivyo
kuwa miongoni mwa wachezaji wanaopewa nafasi kubwa sana ya kuwa mchezaji bora
wa Ligi kuu kwa msimu huu wa mwaka 2014/2015.
Tuzo aliyopta Olivier Giroud inamfanya kuwa
mchezaji wa 16 toka nchini Ufaransa kuweza kutwaa tuzo hiyo katika Ligi kuu ya
soka nchini England.
Miongoni mwa wachezaji wengine raia wa Ufaransa
waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni pamoja na Thierry Henry,Nicolas Anelka,David Ginola,Samir
Nasri,Florent Malouda,Emanuel Petit,Sylvain Wiltod,Louis Saha,Robert Pires na
Erik Cantona.
0 comments:
Post a Comment