WAKATI ikiwaza namna ya kujinasua na kushuka daraja, Klabu
ya Ndanda SC imeamuriwa kumlipa mchezaji Amiri S. Msumi kiasi cha fedha sh.
2,600,000.
Pia Kamati ilihoji mkataba kutokuwa na
kipengele cha mshahara, na kusema ni lazima mkataba uonyeshe Kiasi ambacho
mwajiriwa analipwa.
Pia Kamati imeagiza kuwa vilabu vifahamishwe kuwa fedha
ya kusaini mkataba (sign on fee) hazitakiwi kulipwa kwa mafungu. Tafsiri ya
fedha ya kusaini, ni mchezaji kulipwa fedha yote baada ya kusaini, na si kwa
mafungu.
Pamoja na uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Ndanda
SC ametakiwa kuwepo kwenye kikao cha Mei 3, 2015.
0 comments:
Post a Comment