Wakati wachezaji
wakongwe wa klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania wakiwa wameshawasili
nchini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven, viingilio vya
mpambano huo vimetajwa.
Viingilio hivyo
vimegawanywa katika mafungu matano ambapo VIP A ni shilingi 300,000, VIP B sh.
100,000, VIP C sh. 30,000 wakati jukwaa la Orange itakua sh. 20, Jukwaa la Blue
sh. 10,000 na jukwaa la Kijani ni sh. 7,000.
Tiketi kwa
ajili ya mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya ijumaa asubuhi katika vituo vya
uwanja wa karume, Break Point maeneo ya posta mjini, Dar live Mbagala, Buguruni
Sheli, Ubungo oil com, Makumbusho stand, Feri kigamboni na Feri upande wa
kivukoni, Uwanja wa taifa, Mlimani city, na NPS (National Parking System wa
mjini nao watauza tiketi pia.
Pambano hilo
litafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 11 April katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuanzia saa kumi kamili jioni.
Timu hiyo ya
wakongwe wa Barcelona imeanza kuwasili nchini wiki iliyopita kwa kutangulia kocha
wake Johan Cryuff ambapo baada ya kukamilika walitembelea hifadhi ya Serengeti na
kisha visiwani Zanzibar kwenye mualiko wa rais wa huko Dr. Mohamed Sheni.
0 comments:
Post a Comment