Katibu Mkuu wa TFF
Mwesigwa Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana wenye umri wa
miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.
Akiongea na
waandishi wa habari, Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha vijana
27 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa
kimataifa baadae.
Vijana hawa
mnaowaona hapa wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana nchini,
wakikua na kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini kwa sababu
watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.
Naye Mwenyekiti
wa Kamati ya Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa habari kabla
ya kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha Tanzania
inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.
Mwaka huu
Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA barani
Afrika, nyuma ya Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda vijana
wengi waje kuwa waamuzi wa kimataifa.
Semina hiyo ya
siku 5 inatarajiwa kufungwa ijumaa tarehe 17 Mei, 2015 inajumuisha vijana
kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza, Arusha na Mbeya, kati
ya vijana 37 waamuzi wawili ni wanawake.
Wakufunzi wa
semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.
0 comments:
Post a Comment