Ndoto za
mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Azam Fc kutetea ubingwa wake zimefifia
au kupotea kabisa baada ya hii leo kulazimishwa nyumbani na Mbeya City.
Mchezo wa
ligi kuu ya Vodacom kati ya Azam Fc dhidi ya Mbeya City uliopigwa kwenye uwanja
wa azam Complex umemalizika kwa sare ya goli moja kwa moja.
Azam ndio
waliokua wa kwanza kujipatia bao kunako dakika ya 57 kupitia kwa kiungo wake Michael
Balou, goli lililopatikana kwa juhudi zake binafsi za shuti la umbali wa zaidi
ya mita 25.
Dakika mbili
baadae Mbeya City walipata penalt baada ya Erasto Nyoni kumvuta jezi Dues Kaseke
ndani ya box na mwamuzi kuamuru ipigwe penalt iliyofungwa kiufundi na Rafael Alpha.
Timu zote
mbili zilifanya mabadiliko kwa wenyeji kumtoa Frank domayo na nafasi yake
kuchukuliwa na Amri Kiemba dk 57, Brian Majwega akampisha Faridi Maliki na Gaudence
mwaikimba akachukua nafasi ya Michael Balou.
Kwa upande
wa Mbeya City ambao watajilaumu kwa matokeo hayo baaada ya kupoteza nafasi
mbili za wazi dakika za mwisho, waliwatoa Paul Nonga na Dues Kaseke na nafasi
zao kuchukuliwa na Ahmad Kibopile na Peter Mapunda.
0 comments:
Post a Comment