PRESS
RELEASE
Uongozi wa
klabu wa ya Yanga umebaini upotoshaji na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kanuni
na taratibu za uendeshaji za ligi unaofanywa na baadhi ya viongozi bodi ya ligi
Nchini.
Katika
uchunguzi tulioufanya tumebaini yafuatayo:-
1.
Ukweli
kuhusu kadi za njano alizopata mchezaji wa simba IBRAHIM HAJIB MIGOMBA,mchezaji
huyu tumebaini kuwa alipata kadi nne za njano katika michezo minne aliyecheza
tazama kiambatanisho nyuma ya taarifa hii.
2.
Barua
iliyotolewa na bodi ya ligi nakusainiwa na Kaimu Afisa mtendaji mkuu FATMA
ABDALAH kuidhinisha kuanza kutumiwa kwa kanuni mpya ya kumruhusu mchezaji
husika kuchagua mechi ya kucheza au kutocheza
haikuwa sahihi kutokana na marekebisho hayo kutoanza kutumika.
Tulichobaini
ni kuwa ili mapendekezo ya kanuni hizo yaanze kutumika sheria inataka raisi wa
Tff na katibu mkuu wa Tff kuzisaini ili ziwe rasmi kutumika jambo ambalo
uchunguzi wetu umebaini kuwa raisi wa
Tff bado hajazisaini ili ziweze kutumika japo zimepitishwa na kamati ya
utendeji wa Tff,ili kanunu na taratibu izo zianze kutumika sheria inamtaka raisi na katibu wa Tff kuzisaini ili
kualalisha matumizi yake na si
vinginevyo .
3.
Upotoshwaji
wa taarifa za kuarishwa kwa mchezo wetu na Jkt ruvu ,akizungumza na baadhi ya
vyombo vya habari Kaimu Afisa mtendaji mkuu
wa bodi ya ligi Fatmah Abdala
alikaririwa akisema uongozi wa yanga uliarifiwa kwa barua pepe tangu tarehe 16/02/2015 ukweli katika hili hatukupata taarifa yeyote
ya kuarishwa kwa mchezo wetu na kwa mujibu wa taratibu na kanuni za ubadilishaji
wa Ratiba bodi yaligi inapaswa kukaa na timu husika na kujadili marekebisho ya
mchezo husika jambo ambalo bodi ya ligi haikulifanya wakati wanaarisha mchezo
wetu na Jkt ruvu ambao ulikuwa uchezwe leo .
TUNACHOPENDEKEZA
1.
Shirikisho
la mpira wa miguu TFF kuingilia kati
utata huu kwa kuipokonya klabu ya simba pointi 3 ilizozipata kwenye mchezo wake
na prisons mechi namba 125
2.
Kutoa
adhabu kali kwa viongozi wa simba na mchezaji husika kwa kukiuka kanuni na
taratibu za uendeshaji wa ligi .
3.
Tunamtaka
Kaimu Afisa mtendaji wa bodii Fatmah Abdala ajiuzulu kutokana na kupindisha
sheria na taratibu na pia kupotosha umma wa watanzania kuhusu sheria na pia kwa kutoa kibali hewa
chakuruhusiwa kwa mchezaji HAJIB IBRAHIM Kucheza na prisons uko akiwa na kadi
nne za njano
Imetolewa
Na Idara Ya Habari Na Mawasiliano Ya Yanga
Jerry Murro
CHATI YA MECHI ALIZOPEWA KADI IBRAHIM AJIB
MATCH NO
|
DATE
|
GAME
|
STADIUM
|
17
|
4/10/2014
|
SIMBA
VS STAND UNITED
|
TAIFA
–DAR ES SALAAM
|
99
|
15/2/2015
|
POLISI
MOROGORO VS SIMBA
|
JAMUHURI-
MOROGORO
|
108
|
22/02/2015
|
STAND
UNITED VC SIMBA
|
KAMBARAGE
-SHINYANGA
|
125
|
28/2/2015
|
SIMBA
VS TZ PRISONS
|
TAIFA
–DAR ES SALAAM
|
0 comments:
Post a Comment