Msafara wa watu 25 wa
timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars), unatarajiwa kuondoka
nchini siku ya ijumaa kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza
dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia siku ya jumapili.
Twiga Stars inaanzia
hatua ya pili katika kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Wanawake baada ya
kuwa katika nafasi za juu kwa viwango barani Afrika, na endapo itafanikiwa
kuwaondoa Wazambia itafuzu moja kwa moja kwa fainali hizo.
Msafara utaongozwa na
Blassy Kiondo (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji), Beatrice Mgaya (kiongozi
msaidizi), Rogasin Kaijage (kocha mkuu), Nasra Juma (kocha msaidizi), Furaha
Francis (Meneja), Christine Luambano (Daktari) na Mwanahamis Abdallah (Mtunza
vifaa).
Wachezaji watakokweda
Zambia ni Asha Rashid, Mwajuma Abdallah, Mwanahamis Omar, Donisi Minja, Amina
Bilal, Fatuma Bashiri, Esther Chabruma, Shelda Mafuru, Maimuna Kaimu, Najiat
Abbas, Stumai Abdalla, Fauma Issa, Thereza Yona, Fatuma Hassan, Fatuma Omary,
Sophia Mwasikili, Fatuma Khatibu na Etoe Mlenzi.
0 comments:
Post a Comment