Timu
ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kuodoka
siku ya alhamisi kuelekea jijini Cairo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa
marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa soka la ufukweni
utakaofanyika siku ya jumapili.
Tanzania
inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Misri utakaofanyika
siku ya jumapili jijini Cairo ili kufuzu kwa fainali za soka la ufukweni barani
Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli kufuatia kupoteza mchezo wake
awali uliofanyika Escape 1 jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Msafara
wa timu ya Beach Soccer utakaoondoka na shirika la ndege la Ethiopia,
utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri Mgoyi, kocha mkuu John
Mwansasu, kocha msaidizi Ali Sheikh Alhashby, meneja Deogratius Baltazar na
daktari wa timu Dr Leonidas Rugambwa.
Wachezaji
ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed Rajab Juma, Roland Revocatus Kessy, Samwel
Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi, Mohamed Makame Silima, Mwalimu Akida
Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum Said na Ally Rabby Abdallah.
0 comments:
Post a Comment