Wednesday, March 11, 2015
KOBE BRYANT ATANGAZA KUENDELEA KUCHEZA KIKAPU
Baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu mustakabali wake katika mpira wa kikapu,mchezaji nyota wa timu ya LA Lakers Kobe Bryant amesema kuwa ataendelea kucheza mpira wa kikapu mpaka hapo atakapo amua kustaafu.
Taarifa za kobe Bryant kustaafu zimetokana na kuumia bega mnamo mwezi januari mwaka huu hali iliyomlazimu Kobe kuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima.
Na Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani iliendelea alfajiri ya leo na kushuhudia New Orleans Pelicans ikipata ushindi wa alama 111 dhidi ya Brooklyn Nets.
Cleverant Cavariels nayo ilipata ushindi wa alam 127 dhidi ya 94 za Dallas Mavericks na Lakers wakipata ushindi wa alama 93 dhidi ya 85 za Detroit Pistons.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment