Basi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140
ambalo shirikisho la soka nchini linadaiwa hadi litakapolipwa.
Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya
Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia
mwaka 2007. Hadi sasa tff imeshalipa sh. milioni 70 katika deni hilo.
Tff imesema inafanya jitihada ili kumaliza deni hilo. Pia kuchunguza mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.
0 comments:
Post a Comment