Main Menu

Saturday, January 4, 2014

KOCHA BONIFACE MKWASA AANZA RASMI KIBARUA CHA KUINOA YANGA


Mkwasa (mwenye rangi za Bluu) akiongoza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Bora Mabatini Kjitonyama

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu ya Young Africans jana imeeanza kujifua katika viwanja vya bora Mabatini Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.


Young Africans ilisimama kufanya mazoezi kwa siku takribani tatu kufuatia kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na jana rasmi imeanza mazoezi asubuhi chini ya makocha wasaidzi Mkwasa na kocha wa makipa Juma Pondamali.


Mkwasa alitumia muda wa dakika 5 kuongea na wachezaji wote waliofika mazoezini siku ya jana, kuwaelekeza nini wanapaswa kufanya na kuzingatia mafunzo yake ambapo wachezaji waliweze kutekeleza kwa kiwango cha hali ya juu.


Kocha wa makipa Juma Pondamali aliwafua vilivyo magolikipa Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida" na kusema huu ni mwanzo tu kwani anaamini wachezaji hao watakua katika kiwango kizuri kutokana na uwezo wanaouonyesha katika mazoezi anayaowapatia.


Kikosi cha Young Africans leo kimeendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.


Aidha washambuliaji Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokwenda kwao nchini Uganda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia wanatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki tayari kuungana na wenzao kujiandaa na mzunguko wa pili.

0 comments:

Post a Comment